Ukifika Mkoani Mbeya umefika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe takribani km 70 kutoka katikati ya Jiji la Mbeya.
Rungwe Kuna vivutio vingi yakiwemo Maporomoko ya maji zaidi ya kumi.
Haya katika picha ni maporomoko ya Isabula yaliyopo katika mto Mwalisi mpakani mwa kata ya Matwebe na Kisiba.
Kando ya Maporomoko haya Kuna daraja lililojengwa na Serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Billion 1.6 na kuunganisha kata ya Kisiba na Matwebe.
Watalii wengi hufika hapa na kujionea uoto wa asili unaozunguka mto huu sambamba na kuogelea katika maji huku wakijionea kimo kirefu Cha maji (Dumping level) Cha mwanguko wa maji.
Eneo hili linafaa kwa uwekezaji wa hotel na Makazi ya muda ((campsite) kwa ajili ya kupokea na kuwakaza wageni wanaotiririka takribani mwaka mzima.
Eneo hufikika kupitia Barabara ya Landan - Masukulu, Concil- Masukulu-Kisiba na Kyela-Ipande-Matwebe-Kisiba.
Kando ya mto huu Kuna vivutio vingine yakiwemo Maporomoko ya Mwandambo na Busilya.
Vivutio vingine vilivyopo katika ukanda huu ni Msikiti wa kale zaidi pamoja na Ngome ya Wajerumani iliyopo Kisiba, Ziwa Kisiba , Mti Katembo na maji ya moto yaliyopo kando ya mto Mbaka.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa