Kufuatia Halmsahauri ya Wilaya ya Rungwe kuboresha mazingira mazuri ya uwekezaji, munekano wa ziwa Kisiba umeanza kuvutia na hivyo kuwa eneo pekee lenye mvuto zaidi katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Ziwa hili linalotokana na mlipuko Volkano lipo takribani Km 17 kutoka Tukuyu mjini Barabara ya Masoko-Busokelo na lina kipenyo cha zaidi ya mita 270.
Uwekezaji uliofanywa katika fukwe za ziwa hili (KISIBA CAMPSITE) umeongeza upatikanaji wa huduma ya chakula, malazi, vinywaji, uwanja wa mpira, kuogelea, eneo maalumu kwa ajili ya sherehe kama harusi, na mikusanyiko ya aina mbalimbali.
Ziwa hili lina samaki pamoja na msitu mnene unaozunguka eneo hili na hivyo kumpa mtalii ya kupata upepo mzuri huku akijivinjari katika uoto wa asili sambamba na kujipatia matunda yanayopatikana katika eneo la msitu huu.
Kando ya msitu huu kuna majengo ya kale zaidi yaliyojengwa na enzi za ukoloni wa kijerumani ambayo ilikuwa ngome kuu kabla ya kuhamia Tukuyu mjini.
Aidha kuna Msikiti wa kale zaidi wilayani Rungwe ambao ndiyo chimbuko la misikiti yote wilayani Rungwe na mkoa wa Mbeya kwa ujumla.
Pamoja ha hayo chifu wa kale (Mwakatumbula) na wa Kwanza kumiliki gari katika mkoa wa Mbeya, kupewa nishani ya utawala bora na Malikia Elizabeth anapatikana katika eneo hili katika kitongoji cha Landani ambapo baada ya malikia kuvutiwa na utawala wake eneo la makazi ya chifu llipewa jina linalowakilisha mji mkuu wa nchi ya Uingereza- London.
Makazi ya chifu pamoja na kaburi lake lipo mpaka leo pamoja na zana mbalimbali alizokuwa akizitumia enzi za utawala wake.
Vivuto vingine karibu na ziwa hili ni pamoja na Maporomoko ya maji Isabula, Mwandambo, Busilya, Maji moto Isesero na Mti katembo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa