-KARIBU RUNGWE UWEKEZE NASI-
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imeendelea kuvutia na kuimarisha mazingira ya Uwekezaji ambapo katika hatua hii Kikota /kalongo farm and home iliyopo katika Kijiji Cha Ibula kata ya Kiwira ( Mita chache kutoka newland/ uwanja wa ndege ) wamejenga makazi kwa ajili ya Malazi, Chakula, Vinywaji pamoja na Michezo mbalimbali na hivyo kuwa kati ya vivutio pekee kwa watalii wa ndani na nje ya Mkoa na taifa Kwa ujumla.
Makazi kwa ajili ya Malazi kwa Wageni yapo katikati ya Mashamba makubwa ya parachichi, Ufugaji wa kuku na Mabwawa ya samaki.
Ukiwa hapa unapata fursa ya kuuona kwa karibu zaidi Mlima Mrefu zaidi Nyanda za juu Kusini( Mlima Rungwe) na wa tatu kwa urefu nchini baada ya Milina Kilimanjaro na Meru.
Pia inakupa nafasi ya kufika na kuona Makumbusho ya kabila la kinyakyusa yaliyopo Rungwe Mission, Maporomoko ya maji Malasusa, Kapiki, Daraja la Mungu, Isongole Fishing Camp, Kijungu ziwa Kisiba na Ngosi.
Kairuki , Gerson Msigwa Ngorongoro Conservation Area Authority Ikulu Mawasiliano
Wekeza nasi kupitia Namba +255756462940 email: ded @rungwedc.go.tz Tovuti: www.rungwedc.go.tz
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa