Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vincent Annay ( Wa tatu kutoka kulia walio kaa) ameagiza wakazi wote wa wilaya ya Rungwe kuendelea kutumia fursa zilizopo ili kujiletea Maendeleo na hivyo kujiondoa katika lindi la Umasikini.
Agizo hili limetolewa leo tarehe 23.6.2021 wakati akijitambulisha mbele ya watumishi wa umma ikiwa ni pamoja na makabidhiano kutoka kwa Mkuu wa wilaya aliyekuwepo awali.
Dkt. Vincent anayechukuwa nafasi ya bwana Julius Chalya añayemaliza muda wake amewaalika Watanzania kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya uchumi/viwanda ili kuinua kipato cha wananchi sambamba na uhakika wa soko la mazao yao.
"Mahali pengine mkulima anasukumwa kuja kuchukua mbegu lakini ni tofauti na Rungwe ambapo wakazi wanajituma na kuzalisha Kwa tija"
" Wakazi wa Rungwe wanafuga Ng'ombe, hawaswagi! Hongereni Sana"
Aidha watumishi wameombwa kufanya kazi Kwa bidii, ubunifu na ushirikiano ( Team work) ili kuleta matokeo Chanya ya serikali Kwa watu wake.
Akiaga watumishi na wakazi wa wilaya ya Rungwe , aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Rungwe bwana Julius Chalya ameshukuru Kwa ushirikiano aliopewa Kwa kipindi chote cha miezi 60 aliyoitumikia wilaya hii na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano Mara utakapohitajika.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa