Leo tarehe 6.5.2024 Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu imeendesha kampeni maalumu dhidi ya Usalama wa Watoto Mitandaoni lengo mahususi likiwa ni kuwajengea ustawi bora watoto na kuwaepusha vihatarishi vinavyoweza kurudisha nyuma makuzi stahiki na malezi katika jamii.
Kampeni hii imefanyika katika shule ya Msingi Tukuyu lengo likiwa ni kuzifikia shule 9 zaidi.
Christabela Ngowi ni Afisa Maendeleo Mkuu kutoka katika Wizara hii ambapo ameikumbusha jamii kuhakikisha inawakinga Watoto na Mitandao ya kijamii hasa picha au vielelezo vinavyokinzana na Mila na desturi zetu pamoja na sheria za nchi .
Aidha ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa miongozo ya utoaji wa maudhui Mtandaoni kwani kufanya hivyo itasaidia kuboresha ustawi wa watoto na jamii yote kwa ujumla.
Ngowi ametaja baadhi ya maudhui yasiyofaa mtandaoni kuwa ni pamoja na picha za ngono, matumizi ya madawa ya kulevya, ukatili wa aina mbalimbali , udhalilishaji na vitisho kwa kutumia picha, kumrubuni mtoto mtandaoni, na mengine mengi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa