Mafunzo kwa kamati za shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Rungwe yamezikutanisha kata saba huku yakilenga kuzijengea uwezo kamati hizo namna bora ya Kusimamia vema rasriamali zao, nyaraka za shule, kupanga mipango endelevu ya shule, kusimamia nidhamu ya walimu na wanafunzi ikiwa ni pamoja na kuzuia mimba shuleni, utoro na chakula mashuleni.
Akifungua mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter amesema kuwa ufaulu bora wa wanafunzi unatokana na ushirikiano thabiti kati ya kamati ya shule, walimu, wazazi pamoja na wazazi.
Aidha Bi. Loema amesema kuwa ushirikiano huo ndio utakaoleta mshikamano na kusaidia, ukamilishaji wa miradi ya shule kwa wakati, ikiwa ni pamoja na uwazi wa mapato na matumizi wa fedha za umma.Hata hivyo Bi. Loema amewaomba walimu waliohudhuria mafunzo hayo kutojihusisha na harakati za kisiasa badala yake waendelee kufanya kazi kwa bidii huku wakisubiri siku ya uchaguzi oktoba kwani serikali yao bado inaendelea kuwahudumia wananchi wote akigusia suala la elimu bure jinsi lilivyo kuza ufaulu nchini pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika karibu kata zote.
Pamoja na hayo afisa elimu Msingi bwana Gerald Kifyasi amewaomba wanufaika wa mafunzo hayo kwenda kuyatumia ipasavyo kwani wananchi wana imani nao hivyo ni jukumu lao kwenda kufuta ujinga kwa watoto, kuongeza ufaulu, uwazi pamoja na kulinda rasiriamali za shule.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa