Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Mbeya imefanya ziara na Kukagua ujenzi wa Kituo kipya cha afya kilichopo katika kata ya Kinyala kinachotarajia kugharimu zaidi ya shilingi Million 201 ikiwa ni sehemu ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameishukuru Halmshauri kwa kusogeza huduma ya afya karibu kwa wananchi huku akieleza kuwa kituo hicho kitaondoa changamoto ya kufuata huduma ya matibabu umbali mrefu kwa wakazi wa kata hiyo na wilaya ya Mbeya vijijini.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe.Dk. Vicent Anney ametaja fedha zilizotolewa na serikali ya awamu ya sita kwa hivi karibuni ni kuwa ni pamoja na:
1. Ujenzi wa kituo kipya cha afya kata ya Iponjola -milllion 500
2 Ukamilishaji Zahanati ya Isyonje -million 50.
3.Ukamilishaji Zahanati ya Ilenge -Million 50
4. Upanuzi Kituo cha afya Mpuguso (Ushirika)- Million 50
5. Ukarabati na Ujenzi Hospitali ya wilaya Tukuyu (Makandana) -Billion 1
VItuo vingine vinavyoendelea na ujenzi kwa hatua nzuri ni pamoja na kituo cha afya kata ya Kyimo (Milion 500), Kituo cha Afya Kata ya Ndanto- Tozo ya miamala ya simu ( Million 250)
Hatua hii ya Serikali inatarajia kuondoa na kutokomeza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya afya kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa