Leo tarehe 14.4.2025 Kamati ya Siasa Wilaya ya Rungwe ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe Bwana Mekson Mwakipunga imefanya ziara na kukagua miradi ya Maendeleo iliyotekelezwa katika robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2024/25.
Pamoja na Wajumbe wengine Ziara hii imehudhuriwa pia na Kamisaa wa Chama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe Jaffar Haniu.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na ujenzi wa Mabweni Mawili katika shule ya sekondari Wasichana Kayuki, Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa kutumia mapato ya ndani katika shule ya msingi Masebe, Ujenzi wa shule Mpya ya amali katika kata ya kisondela pamoja na Shule mpya ya sekondari kata ya Kawetere.
Miradi yote imegharimu zaidi ya shilingi Billion 1.5
Kamati imeridhishwa na kiwango cha ujenzi kilichofikiwa huku ikimpongeza Rais Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuimulika Wilaya ya Rungwe na kuilpatia miradi mkakati itakayosaidia kutatua changamoto za wakazi wa wilaya ya Rungwe.
Pamoja na miradi hii, Pia Rais ameidhisha fedha na kuipatia Wilaya ya Rungwe kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ghorofa mbili Hospitali ya wilaya Tukuyu (Billion 2) Kituo cha afya Masoko na Kiwira (Billion 1), Upanuzi wa shule ya sekondari Rungwe na Lupepo, Barabara ya Ndulilo -Itete na Katumba- Lupaso kwa kiwango cha Lami pamoja na miradi ya maji na umeme.
Huu utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa wakazi wa wilaya ya Rungwe.
Renatus Mchau
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Atubonekisye Mshani
Ikulu Mawasiliano
Bunge la Tanzania
CCM Tanzania
CCM MKOA WA MBEYA
Kenny Lawrence
JamiiForums
Tanzania Investment Centre
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa