Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe Mh.Sam Mwakapala alipokuwa akitoa neno la ukaribisho katika kikao cha Chama cha Mapinduzi kilichofanyika mjini Tukuyu katika ukumbi wa Landmark Hotel tarehe 18/12/2018. Mwenyekiti alitoa pongezi kwa usimamizi mzuri wa miradi hiyo yenye tija katika Halmashauri, usimamizi huo mzuri na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Halmashauri na Chama cha Mapinduzi. Alisema kamati ya Siasa ilipokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi waliyoifanya tarehe 15/12/2018 na 16/12/2018.
Pia Mwenyekiti huyo alisisitiza wataalamu wa Halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kusimamia vizuri miradi hiyo. Aidha katika Kikao hicho alishauri viwango vya mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu viongezwe ili waweze kufanya shughuli kubwa zaidi kwa kiasi hicho. Kikao hicho kilikuwa ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya 2015, taarifa hiyo ilitolewa na Mkuu Wa Wilaya ya Rungwe Mh.Julius Challya.
Katika kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dk.Tulia Akson Mwansansu, Wabunge wa majimbo yote ya Wilaya ya Rungwe wajumbe wa kamati za Chama cha Mapinduzi toka katika Kata mbalimbali.Katika kikao hicho pia wakuu wa Idara za Halmashauri za Wilaya za Rungwe na Busokelo ,menejawa TRA (W), Wakuu wa Vyuo vya Ualimu Vilivyopo Wilaya ya Rungwe,Meneja wa TANESCO, Meneja wa TARURA (W)Kamati ya Ulinzi na Usalama (W).
(Pichani ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Rungwe waliovaa Sare za Chama na Wakuu wa Idara za Halmashauri za Wilaya Rungwe na Busokelo)picha na Suzan Mhoja
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa