Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano na Amani Tanzania Dkt Alhad Juma Salum amefanya ziara katika Wilaya ya Rungwe ambapo pamoja na mambo mengine amehamasisha zoezi la Upandaji miti pamoja na uchangiaji damu kwa wagonjwa
Zoezi hili linafanyika nchi nzima na kilele chake kitakuwa kesho tarehe 6.3.2024 katika jiji la Mbeya.
Katika Mkoa Mbeya jumla ya miti 2400 imepandwa na jumuiya hii katika Halmashauri saba (7) huku Halmashauri ya Rungwe pekee ikipanda jumla ya miti 750.
Dkt Salum amewahamasisha Wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kuchangia damu, kwani damu haichagui dini na wala mhudumu wa afya haulizi dini ya mtu kabla ya kutoa msaada wa damu ya ziada.
Aidha amewakumbusha Watanzania kuendelea kuheshimiana, kuvumiliana na kulinda amani iliyopo kwani kufanya hivyo kutasaidia kuleta utulivu na maendeleo katika jamii.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa