Kamati ya Lishe ya Halmashuri ya Wilaya ya Rungwe, imekaa kikao hii leo kujadili utekelezaji wa shughuli za lishe Wilayani Rungwe.
Akiongoza kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Rungwe Bw. Castory Makeula, ambaye ndiye aliyekuwa Mwenyekiti wa kikao akiwa pamoja na wadau mbalimbali wa lishe wamechambua kwa pamoja utekelezaji wa shughuli mbalimbali za lishe.
Katika uchambuzi wa taarifa hizo, pamoja na kujiwekea mikakati mbalimbali ya kuimarisha upatikanaji wa chakula mashuleni imeonekana kuwa sasa hali inaendelea kuimarika na sasa utoaji wa chakula mashuleni unapatikana kwa 63% kutoka 30% kwa upande wa shule za sekondari na 43% kutoka 16% kwa upande wa shule za msingi katika kipindi cha miezi 3 pekee.
Hata hivyo kikao hicho kimeazimia kuwa hali bado hairidhishi na jitihada za makusudi zinapaswa kuongezwa ili kutoa hamasa kwa jamii kuweka kipaumbele cha utoaji wa chakula kwa wanafunzi ili kuwajengea uwezo wa kuhimili na kuongeza ufaulu wa masomo yao.
Wakichangia katika kikao wadau hao wameishauri idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ya Wilayani Rungwe kuwaongoza katika kalenda ya mazao kulingana na msimu, ili iwasidie kupanda mazao ya lishe wakati wote kwani hali ya hewa ya Rungwe inaruhusu kulima majira yote ya mwaka.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa