Kamati ya Lishe Wilaya ya Rungwe imepongeza maafisa Ugani katika kata zote 29 kwa kuendelea kutoa elimu juu ya kilimo bora cha mahindi lishe na maharage lishe sambamba na na namna bora ya mbinu bora ya uvunaji na uhifadhi ili kuzuia sumu kuvu ambayo ni hatari kwa afya ya mlaji.Wilaya ya Rungwe ipo katika msimu mkubwa wa uvunaji wa mahindi huku mvua ikiendelea kunyesha ambapo kushindwa kutunza vizuri mahindi hayo kunapelekea kuoza na hivyo kuwa katika mazingira ya kupata sumu kuvu.
Kwa Mujibu wa shirika la Research to nourish Afrika linataja kuwa Sumu kuvu ni sumu zitolewazo na aina ya ukungu kuvu (fangasi) unaoota kwenye mbegu za nafaka na jamii ya kunde, mazao ya mizizi, karanga, vyakula na malisho ya wanyama vikiwa shambani au kwenye ghala. Ingawa aina nyingi za kuvu zinaweza kuota na kukua katika vyakula hivi, ni wachache tu amabao hutoa sumu kuvu. Endapo vayakula anavyokula binadamu au mnyama vina sumu kuvu nyingi afya zao hudhurika kwa kiwango cha juu. Sumu kuvu haionekani kwa macho, haina harufu, haina kionjo, wala rangi, lakini kuvu anayetoa sumu hizo anaweza kuwa na rangi ya kijani, chungwa, kijivu au njano chafu na anaweza kutoa harufu ya uvundo. Karibia asilimia 25 ya vyakula ulimwenguni vina maambukizi ya sumu kuvu na watu bilioni 2.5 wako katika hatari ya kudhurika.
HATARI ZITOKANAZO NA SUMU KUVU
tafiti wa shirika la IITA unataja kuwa: Kama chakula au kinywaji chenye sumu kuvu kitatumiwa na binadamu au mnyama ataugua kwa kutegemea na kiasi cha sumu kuvu kilichomo. Vyakula ambavyo vinaweza kuambukizwa sumu kuvu ni kama vile mahindi na unga wake, karanga na mazao yanayotokana na karanga, muhogo, nyama, mayai na maziwa (vitokanavyo na mnyama au ndege aliyeambukizwa pamoja na mazao yao) na vyakula vya mifugo (vyenye mbegu zilizoambukizwa au nyasi au vyaluka vya mifugo vya kutengenezwa). Saratani, hasa ya ini, kushusha kinga ya mwili, kudumaa hasa kwa watoto, sumu kwenye figo na vifo kwa binadamu na wanyama ikiwa viwango vya sumu kuvu ni vikubwa. Baadhi ya sumu kuvu hutoka kwa mama kwenda kwa mtoto akiwa bado tumboni. Kutokana na madhara ya afya yanayosababishwa na sumu kuvu kwa binadamu na wanyama sumu kuvu haziruhusiwi kuwepo katika mazao yaliyokusudiwa kwa biashara na kama zikigunduliwa katika mazao ya kilimo hayatauzika na badala yake yatateketezwa. Kwa kiwango kikubwa sumu kuvu huathiri biashara, faida na afya za wazalishaji.
NJIA ZA KUZUIA SUMU KUVU-
-Lima aina za mazao zenye ukinzani dhidi ya kuvu wanaotoa sumu kuvu (kama aina hizo zinapatikana)Vuna mazao yakiwa yamekauka vizuri kama inavyoshauriwa na bwana/bibi shamba na epuka kutia majeraha kwenye mazao yako
- Usianike mazao yako kwenye udongo mtupu. Anika sehemu iliyoinuka kama meza na utumie turubai au aina nyingine ya kifaa cha kuanikiaWakati na baada ya kuvuna tupa mbegu au mazao yaliyoozaHifadhi mazao mahali pakavu na pasipo na joto.
- Hakikisha mazao yaliyohifadhiwa hayalowiGhala liruhusu mzunguko wa hewa,
-zuia wadudu waharibifu na kuvu kwa kunyunyiza madawa yaliyokubalika na kushauriwaTumia madawa yanayodhibiti na kuondoa sumu kuvu wakati wa usindikaji wa vyakula vya binadamu na vile vya wanyama
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa