MUHTASARI WA HOTUBA YA MH. RAIS DR. SAMIA SULUHU HASSAN WAKATI WA UZINDUZI WA DIRA YA TAIFA 2050 UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE DODOMA 17.7.2025
1. Pongezi kwa wote walioshiriki katika maandalizi ya dira wakiwemo wastaafu ambao wamekuwa wakifuatilia, mchakato huu tangu mwanzo. Pongezi za pekee kwa Mh Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango kwa kuasisi na kuzindua uandishi wa mpango na kwa mwongozo wa mara kwa mara.
2. Dira imeandikwa kwa kuzingatia mambo mengi muhimu yakiwemo yafuatayo:
i. Tanzania ni tajiri wa rasilimali. Wajibu wa viongozi ni kubuni, kuibua mipango na kuhakikisha nchi inapiga maendeleo ya kiuchumi kuwanufaisha wananchi kutokana na rasilimali zao
ii. Tanzajia ni Taifa lenye umoja, amani na Mshikamano. Ustawi huu wa nchi yetu umekuwa tunu kubwa katika kuwawezesha wananchi kutekeleza shughuli zao bila ubabaifu. Awamu zote sita zimejikita kuboresha maisha ya wananchi kwa mioango kadha wa kadha iliyosukumwa kwa kauli mbiu mbalimbali na hatimaye Tanganyika ya 1961 ni tofauti sana na Tanzania ya 2025.
iii. Misaada na mikopo haiwezi kuwa Msingi wa maendeleo bali kichocheo tu. Lazima kujenga misingi ya kujitegemea kwa kutumia rasilimali za Taifa letu wenyewe.
iv. Ushiriki. Sote tushiriki kwenye utekelezaji wa Dira hii hatua kwa hatua kuanzia lengo Kuu, shabaha, Malengo mahusus hadi viashiria vya mafanikio. Jitihada za pamoja zinahitajika kutimiza yaliyomo katika dira hii.
3. Dira imezingatia mahitaji ya sasa yakiwemo ***mabadiiliko ya mfumo wa uchumi ili kuakisi matumizi ya teknolojia ya hali ya juu,
*** Mabadiliko ya Tabia nchi
*** Mabadiliko ya kidemografia hasa kwa kuzingatia matamanio ya kundi kubwa la vijana, sekta binafsi
*** mabadiliko katika teknolojia ya akili inayotoa kipaumbele kwenye matumizi ya akili Mnemba
*** Tujielekeze katika kutekeleza yaani kutenda zaidi kuliko kusema. Mtihani halisi wa dira hii ni katika utekelezaji.
4. Dira imezingatia tisa za viapumbele. Kupanga ni kuchagua hivyo sekta za kipaumbele zilizozingatiwa ni pamoja na:
Kikimo
Utaliii
Viwanda
Ujenzi
Uchuki wa bkue
Fedha
Michezo n.k
5. WITO NA MAELEKEZO YA MH. RAIS DR. SAMIA SULUHU HASSAN
a. Tubadilike kifkira na kimatendo. Tume iweke vigezo vya utendaji kupitia ofisi ya Waziri Mkuu utendaji upimwe
b. Mabadiliko ya Sera na Sheria. Tume ya kurekebisha sheria iainishe maeneo yanayohitaji maboresho kwenye mfumo mzima wa Sera, Sheria na kanuni mbalimbali kuwezesha utekelezaji wa dira.
c. Mfumo wa ufuatiliaji na Tathmini uimarishwe. Uratibu wa utekelezaji uzingatie mshikamano wa kiserikali hadi kwenye sekta binafsi. KPI ziandaliwe kwa vigezo vya utendaji kulingana na shabaha za dira
d. Sekta binafsi ishiriki kikamilifu katika utekelezaji. Uwekezaji, ubunifu na upanuaji wa wigo wa ajira pamoja na mifumo jumuishi ya utendaji kwa tija ya Taifa
e. Uwepo Mkakati wa mawasiliano, elmu kwa umma ili wadau wote waielewe dira
f. Kulinda haki na maadili. Mahakama na taaisis zote za kutoa haki zitimize wajibu bila uolpendeleo. Taasisi za kijamii zikiwemo za dini zishiriki kuimarisha ustawi wa jamii kwa kusimamia misingi ya maadili
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa