Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya ukaguzi wa Serikali za Mitaa Mhe. Boniface Butondo (MB) ameiongoza leo tarehe 22.03.2022 kamati yake kukagua mradi wa ujenzi na ukarabati wa Shule ya Wavulana Rungwe.
Katika ukaguzi huo kamati hiyo imepongeza na kuridhishwa na hatua nzuri iliyofikiwa katika mradi huo na kuwa sasa wanafunzi watapata fursa nzuri ya kusoma kwa bidii na na kupata mafanikio makubwa.
Ukarabati wa shule hii kongwe nchini (1961) ulianza mapema mwaka 2020 na mpaka sasa umekalika na kuanza kutumika.
Mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi Million 752 ambapo imejumuisha ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa na mabweni pamoja na jengo la utawala.
Fedha zimetolewa na Serikali Kuu.
Mbele ya wanafunzi, kamati hiyo imewaagiza wanafunzi kutunza miundombinu ya shule hiyo na kuhakikisha wanailinda ikiwa ni hatua nzuri ya kuhakikisha juhudi zilizofanywa na serikali ya awamu ya sita dhidi yao wanazithamini.
Shule ya Sekondari Rungwe hudahili wanafunzi wa kidato cha tano na sita tu kwa tahasusi ya HGL, HKL, HGK, PCM, PCB, CBG, HGE na EGM na ina wanafunzi zaidi ya 400.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa