Kamati ya Uongozi na Serikali za Mitaa ya Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania leo tarehe 15.03.2022 ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Abdala Chaurembo (MB) Mbele ya Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Inocent Bashungwa imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe na kukagua barabara ya kiwango cha Lami (MASEBE-LUTETE KM 7 na MPUGUSO- BUGOBA KM 5).
Katika Ziara hiyo kamati imepongeza ujenzi wa barabara hiyo kwani kwa kufanya hivyo wakazi wa kata ya Mpuguso, Ilima na Kisondela wamefunguliwa fursa ya kiuchumi sambamba na ustawi wa jamii katika utoaji wa huduma ya afya, elimu, kilimo, ufugaji na uwekezaji katika sekta ya Viwanda.
Aidha Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Inocent Bashungwa ameileza kamati hiyo kuwa Serikali Kupitia TANROAD ipo mbioni kukamilisha kipande cha Mita 800 kilichobaki kuanzia Ushirika mpaka Shule ya Msingi Masebe ili kuifanya barabara hiyo kupitika kwa urahisi kwa zaidi ya km 8.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Homera ameieleza kamati hiyo kuwa barabara zote zinazojengwa kwa kiwango cha lami imeelekezwa kuwekewa taa za barabarani ili kuongeza usalama wa uraia na mali zao wakati wa usiku na tayari baadhi ya miji maelekezo hayo yameanza kutekelezwa.
Barabara ya Masebe- Lutete- Bugoba imejengwa na Wakala wa barabara vijijini (TARURA) kwa msaada wa Umoja wa Ulaya (EUROPEAN UNION) na imegharimu zaidi ya shilingi Billion 2.5.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa