Wakazi wa kijiji cha Lubanda kata ya Ilima wameazia kupanda miche isiyopungua 50 ya zao la kakao kwa kila kaya ikiwa ni sehemu ya kuongeza kipato sambamba na kuondokana na umasikini.
Mbele ya Mkuu wa wilaya ya Rungwe, Mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Wema Mwakibibi ametaja kuwa tayari kila zoezi hilo limenza kutekelezwa kwa miaka miwili iliyopita ha hivi karibuni wataanza kunufaika huku maaafisa ugani wakiendelea kuwapa ushauri wa kitaalamu kwa ukaribu zaidi.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney ameagiza wakazi wa kata hiyo kuanza kuunda vikundi vya uchakataji na usindikaji wa zao hilo ikiwa ni hatua ya kuliongezea thamani na kupanua wigo wa biashara ya kakao nchini.Katika nchi ya Tanzania zao hili hulimwa kwa wingi katika Wilaya ya Rungwe, Kyela na Busokelo.
Wakati huo huo Dkt Anney amewakumbusha wakazi wote wa wilaya ya Rungwe kuendelea kijiandaa na zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajia kutekelezwa agosti 23 mwaka huu na kuipa serikali nafasi ya kupanga mipango endelevu ya maendeleo kwa watu wake.
Aidha amekemea vitendo vya mauaji vinavyozidi kushamiri katika maeneo mbalimbali ambayo vinazidi kuuondoa hali ya utulivu katika wilaya hii huku akitaja chanzo kikubwa kuwa ni migogoro ya ardhi.
FUNGUA KIUNGANISHI HIKI KWA HABARI ZAIDI
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa