Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney amewatembelea na kuwajulia hali wagonjwa katika hospitali ya wilaya Tukuyu (Makandana) huku akiweka jiwe la msingi katika jengo la mama na Mtoto lililopo katika hospitali hiyo.
Jengo hilo lililogharimu kiasi cha shilingi million 481 lina jumla ya vyumba 42 vya kutolea huduma na tayari jengo hili limeanza kufanya kazi.
Aidha Mhe Anney amearifu kuwa serikali inaendelea kuboresha huduma za afya katika maeneo mbalimbali ambapo katika hatua hii hosipitali inatarajia kupokea kiasi cha shilingi Billion Moja ikilenga kuboresha majengo na miundo mbinu mingine.
"Ndugu zangu kabla ya jengo hili jipya kujengwa akina mama walikuwa wanalala chini lakini baada ya Serikali kutoa kiasi kikubwa cha pesa sasa mama zetu wanalala mahali salama mpaka vitanda vinabaki. Hii ni kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya Mama yetu Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na utekelezaji mkubwa wa ilani ya Chama cha Mapinduzi". Amewakumbusha watanzania.
Pamoja na hayo ameeleza kuwa serikali inaendelea kupeleka madawa pamoja na vifaa tiba katika hospitali hiyo sambamba na vituo vya kutolea huduma ya afya vijijini ili kuwajengea afya stahiki wananchi na hivyo kushiriki katika shughuli za maendelea ipasavyo.
Katika hatua nyingine wananchi wameagizwa kujiunga na bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) ili kupata fursa ya matibabu katika maeneo mbalimbali nchini kwa gharama nafuu.
Get More Messages for Rungwe District Council
You can add a Messenger button to your post to get more messages for Rungwe District Council.
0
People Reached
17
Engagements
17 Shares
Like
Comment
Share
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa