Serikali ya awamu ya sita imetoa jumla ya shilingi Million 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa pamoja na samani zake kwa shule ya msingi Ipyana iliyopo kijiji cha Simike kata ya Lufingo.
Huu ni utekekezaji mkubwa wa ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ikiwa ni dira thabiti ya maendeleo nchini.Vyumba kama hivyo vinajengwa pia katika shule ya msingi jumuishi ya Katumba II ambapo ujenzi upo katika hatua ya upauaji.
Aidha serikali imetoa jumla ya shilingi million 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari Msasani katika kitongoji cha Bulongwe barabara ya Tukuyu- Lufumbi Masoko ambapo kukamilika kwake kutagharimu kiasi cha shilingi million 600.
Ujenzi wake umefikia asilimia 80%.Aidha shule ya sekondari Suma imepokea zaidi ya shilingi million 90 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala na vyumba vya madarasa. Ujenzi upo hatua ya upauaji.
Ikumbukwe kuwa kupitia mpango wa COVID 19 mwishoni mwa mwaka uliopita (2021) Serikali ilitoa jumla ya shilingi Billion 1.1 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 55 vya madarasa katika shule za sekondari hali iliyoondoa msongamano madarasa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Ilani imeendelea kutekelezwa katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, maji, barabara, umeme, kilimo, ufugaji, utalii na stahiki kwa watumishi wa umma.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa