KYOBO KITUO BORA CHA KAZI
Katika kuboresha makazi ya watumishi wake, serikali imetoa kiasi cha shilingi Million 114 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba mbili za walimu katika shule ya sekondari KYOBO iliyopo kata ya Ikuti.
Shule hii yenye kidato cha kwanza na pili ipo takribani KM 10 kutoka Ikuti makao makuu ya Kata.
Nyumba hizi zitakapokamilika zitakuwa na uwezo wa kuhudumia familia nne.
Aidha kijiji cha KYOBO kimepokea fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa nyumba ya mtumishi wa afya katika Zahanati ya kijiji hicho.
Pamoja na kufikishiwa Mradi wa umeme na maji, kijiji cha Kyobo kimejengewa barabara yenye urefu wa KM 07 na Wakala wa barabara Mjini na Vijijini (TARURA) kutoka Kijiji cha Ibungu mpaka Zahanati ya Kyobo/ Kyobo sekondari na Shule ya Msingi.
Kijiji cha Kyobo ni maarufu kwa kilimo cha Iliki, Kahawa , Nanasi, Mbao na Ndizi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa