Baada ya hostel ya shule ya sekondari Nkunga kuungua Kwa moto mapema Jana alfajiri ( January , 27) wadau mbalimbali wamejitokeza kuchangia ujenzi wa hostel mpya inayotarajia kugharimu kiasi cha shilingi million 113 na kulaza wanafunzi wapatao 80.
Akikabidhi misaada hiyo Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mheshimiwa Julius Chalya amearifu kuwa kiwanda cha maji Tukuyu kimetoa jumla ya mifuko ya saruji 250 huku kampuni ya majani ya chai MeTL ikitoa mifuko 100 ya saruji.
Aidha ofisi ya Mbunge jimbo la Rungwe imetoa msaada wa fedha taslimu kiasi cha shilingi million 2 huku umoja wa wakuu wa shule ukitoa ahadi ya kununua magodoro yote yatakayotumiwa na wahanga hao. Pamoja na hayo idara ya elimu sekondari itanunua madaftari yatakayotumika kujifunzia darasani.
Akitoa salamu za pole Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mheshimiwa Mpokigwa Mwankuga amesema kuwa hostel hiyo itarajiwa kukamilika ndani ya miezi mitatu huku akiomba wadau mbalimbali kuendelea kuchangia misaada mbalimbali na kuonya watendaji kutothubutu kutumia misaada hiyo vibaya ikiwa ni pamoja na kulipana posho.
Pamoja na hayo Mkurugenzi MTENDAJI halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bi. Loema peter ameomba wakazi wa kata ya Nkunga kuanza kuchimba msingi wa jengo hilo pamoja na kukusanya mchanga ili ukamilishaji wa jengo hilo ufanyike mapema na kuwapa fursa wanafunzi hao kupata malazi salama.
Hostel hiyo iliyokuwa inakaliwa na wanafunzi wa kike tu, na Kwa sasa wamerudishwa nyumbani mpaka siku ya jumatatu ijayo februari mosi. Wakirejea watatumia sehemu ya madarasa kwa ajili ya malazi huku wakisubiri ujenzi wa hostel mpya.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa