Barazani leo tarehe 29.04.2022 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga ametaja kuwa katika kipindi cha robo ya tatu mwaka 2021/2022 January, February, na March mwaka huu, Halmashauri imekusanya jumla ya Tsh. 1,375,385,534.36 sawa na asilimia 104% ya Makisio ya Shilingi 1,326,564,689.00 kwa kipindi hicho cha miezi mitatu.
Aidha ameeleza kuwa kuanzia mwezi Julai 2021 Mpaka Machi 2022 Halmashauri imekusanya jumla ya shilingi 4,061,614,477.40 sawa na asilimia 77% ya makisio ya mwaka ya Shilingi 5,306,258,756.00
Mapato hayo yametokana na vyanzo kama ushuru wa mazao, ada ya ushuru, ada ya leseni, Mpato kutokana na mali za Halmashauri, Ushuru wa mali asili, Mapato ya hisa na ada za shule na ICHF.
Mapato hayo yamesesaidia katika ujenzi wa miradi ya kutolea huduma za afya (Kituo cha afya Kinyala), elimu na matumizi mengine ya Serikali.Katika mapato hayo ada za shule zimekusanywa kwa asilimia 91%, Mali asili 86% na Mazao 80% Mapato mengineyo 159%
Mafanikio katika makusanyo hayo yametokana na usimamizi mzuri sambamba na ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi.
Mhe. Mwankuga ameeleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/22 Halmashauri imepata HATI SAFI ya ukaguzi wa mahesabu na hali iliyotokana na ushirikiano mzuri kati ya Madiwani, Chama na Serikali, pamoja na watalamu.
Pamoja na hayo Mwankuga amebainisha kuwa katika kipindi cha miezi mitatu Halmashauri imepokea shilingi Million 290 kutoka serikali Kuu, fedha zilizotumika kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Ipyana, Katumba, Shule ya sekondari Suma na ukarabati jengo la Mamlaka ya mji mdogo Tukuyu.
Miradi mingine ni ujenzi wa Kituo cha afya Iponjola (Million 500), Ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharula hospitali ya Wilaya Tukuyu (Million 300), Ukarabati na ujenzi wa majengo mapya Hospitali ya wilaya Tukuyu (Billion 1)
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa