Ofisi ya Rais- TAMISEMI inao utaratibu wa kutoa taarifa ya mapato na Matumizi ya ndani ya Halmashauri kwa kila robo mwaka ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika Ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri nchini.
Katika robo ya nne mwezi Julai mwaka huu TAMISEMI iliandaa taarifa ya mwaka ya mapato na Matumizi ya mapato ya ndani ya kila Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Pamoja na mambo mengine taarifa ilianisha vigezo vilivyotumika kupima ikiwa ni nyenzo mahususi ya kuongeza uwajibikaji,uwazi sambamba na utawala bora.
Vigezo hivyo ni pamoja na Ukusanyaji wa mapato ya ndani, Matumizi ya mapato hayo kwenye miradi ya maendeleo, usimamizi wa mikopo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya ndani, utekelezaji wa mapendekezo ya CAG na mwisho namna Halmashauri zinavyoimarisha utawala bora kwa kuhabarisha umma juu ya shughuli mbalimbali zinavyotekekezwa na Serikali.
Katika tathimini ya jumla Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilipata alama 86.6 sawa na daraja "A" ikishika nafasi ya 8 kati ya Halmashauri 184 ikiongozwa na Halmashauri ya Mbulu iliyopata alama 89 huku Halmashauri ya Liwale na Chato zikisalia na na alama 48 na kushika nafasi za mwishoni.
Mathalani kwa mwaka fedha uliopita 2021/22 Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilikusanya jumla ya shilingi Billion 5,486,943,286.55 ambayo ni sawa na asilimia 103% ya makisio ya ndani ya mwaka ya TZS 5,306,258,756.00Fedha hizi zilisaidia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama Ukamilishaji wa kituo cha afya Kinyala, ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya Msingi Lyebe,Ilima, Kinyika, pamoja na Sekondari ya Masukulu na Kyimo.
Ukarabati wa nyumba mbili za watumishi, kurejesha asilimia 20% za makusanyo ngazi ya kata, ukarabati wa machinjio ya Ndaga, Ibighi na Tukuyu na Ibililo.Aidha Mapato ya ndani yametumika kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji katika soko la Mpuguso, Tandale na Mabonde na ukarabati pamoja na uwekaji wa mifumo ya kukusanyia mapato katika jengo la mamlaka ya mji mdogo Tukuyu.
Shughuli zingine ni pamoja na kuunga mkono juhudi za wananchi mathalani ukarabati na ujenzi wa stendi ya daladala Tukuyu mjini, soko la Wamachinga, daharia shule ya sekondari Nkunga, kukodi grader kusawazisha eneo la ujenzi shule mpya ya sekondari Msasani, na ukamilishaji wa choo kituo cha afya Mpuguso.
Hata hivyo Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu waliingiziwa kwenye akaunti zao kwa kutumia akaunti za vikundi ( Mkopo usio na riba) jumla ya shilingi Million 321 ikiwa ni asilimia kumi ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Katika tathimini hiyo Halmashauri ilifanikiwa kuhabarisha watu wake kwa asilimia 67% na kushika nafasi ya kumi kati ya HALMASHURI 184 nchi nzima.
Mafanikio haya yamewezekana na kufikiwa kutokana na ushirikiano mkubwa kati ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, Baraza la Madiwani, Menejimenti, Watumishi na Wananchi kwa ujumla.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa