HALMASHAURI YA WILAYA YA RUNGWE YAPATA HATI SAFI YA UKAGUZI
Imefahamishwa kuwa umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi wa umma ndiyo njia pekee itakayosaidia halmashauri yeyote kupata hati safi ya ukaguzi na hivyo kuleta taswira chanya kwa wananchi wake.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila wakati akihutubia kikao cha Baraza la madiwani (baraza la kujadili hoja za mkaguzi wa nje) lililofanyika katika ukumbi wa chuo cha ualimu Tukuyu ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kupata hati safi kwa msimu wa 2018/19.
Aidha mh. Chalamila amewaomba watalaamu wa halmashauri hiyo kuendelea kuwa wakali wakati wa ukusanyaji wa mapato huku akisistiza kuwa vikundi vyote vilivyopata mikopo ya halmashauri na kushindwa kurejesha kwa wakati vipelekwe mahakamani ili fedha hizo ziweze kutumika kuwakopesha wanufaika wengine.
Pamoja na hayo Mh. Chalamila ameupongeza utawala wa halmashauri hiyo kwa kusimamia miradi ya maendeleo kwa ufanisi mkubwa huku akimpa kongole Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter kwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa jengo la mama na mtoto lililopo katika hospitali ya wilaya Tukuyu ambalo mpaka mpaka sasa sehemu ya jengo hilo imenza kutumika.
UGONJWA WA CORONA
Akizungumzia maambukizi ya ugonjwa wa corona Mhe. Chalamila ameomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kuwa watulivu huku wakiendelea kuchukua tahadhari zinazostahiki.
“Ugonjwa huu hauchagui rangi wala kipato cha mtu ndiyo maana siyo rahisi kusikia mgonjwa akiomba akatibiwe nje ya nchi kote kumeshindikana” alisisitiza.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa