UKIFIKA RUNGWE USISAHAU KUFIKA ENEO TULIVU ZAIDI
Ukifika Isongole fishing camp iliyopo kijiji cha Unyamwanga kata ya Isongole ni moja ya maeneo yenye mvuto wa pekee.
Eneo hili linalomilikiwa na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa sasa limepata mwekezaji hatua iliyoboresha mandhari na mwonekano wa kambi hiyo ya wavuvi iliyojengwa mwanzoni mwa miaka ya 1900.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau ametoa maelekezo kwa mwekezaji wa eneo hilo kukamilisha kwa wakati upanuzi wa eneo hilo ili wakazi wa wilaya ya Rungwe na Tanzania kwa ujumla waanze kunufaika na uwekezaji kwa kupata chakula, malazi, kupiga picha, na uvuvi.
Hatua hizi pia itawezesha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri.
Awali katika eneo hili yalikuwa makutano ya watawala wa Kijerumani kutoka kona zote za maeneo ya Rungwe na Mbeya mjini kwa ajili ya Shughuli za starehe hasa mwishoni wa juma.
Isongole fishing camp(IFC) ipo umbali wa takribani km 7 kutoka Idweli (Namba one) na inapatikana kando ya mto Kiwira.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa