Kamati ya fedha (FUM) imefanya ziara na kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Kiwira kilichopo katika Kijiji cha Mpandapanda kata ya Kiwira.
Serikali imetoa kiasi cha shilingi million 500 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki.
Jumla ya majengo matano yanatarajiwa kujengwa katika kituo hiki likiwemo la Wagonjwa wa nje, Maabara, Mama na mtoto pamoja na jengo la kufulia.
Awali Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan alipofanya ziara katika wilaya ya Rungwe mwaka 2022 alitoa kiasi cha shilingi million 10 kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki ikiwa ni sehemu ya Kuunga nguvu za Wananchi wa Kiwira.
Aidha Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa kutumia mapato yake ya ndani imetoa kiasi cha shilingi million 10 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huu pamoja na vifaa vya ujenzi kama mbao na vingine vingi.
Huu ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha watanzania wanapata huduma nzuri na stahiki karibu na makazi yao.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa