Ukiwa na kadi ya bima iliyoboreshwa (ICHF) unapata uhakika wa kupata matibabu katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali vilivyotapakaa nchi nzima.
Ni kwa gharama ya shilingi 30,000/= wanufaika wapatao 06 hupata huduma hiyo muhimu kwa maisha ya binadamu.
Watalamu wa usajili wameenea katika vijiji vyote katika wilaya ya Rungwe pamoja na Ofisi ya Mratibu wa mfuko huo iliyopo Mamlaka ya Mji Mdogo TUKUYU.
Wasiliana na Mtendaji wa kijiji kwa maelezo zaidi dhidi ya Afisa usajili katika eneo lako unaloishi.
ICHF ina faida kubwa, zaidi ni kumhakikishia mgonjwa uhakika wa matibabu mwaka mzima .
Kuna wakati mtu hukosa hata pesa ya kununulia Mahitaji ya kila siku, lakini uwepo wa bima hii umerahisisha maisha na utendaji wake.
Mbumi Lwangalo mkazi wa Kata ya Masukulu amenufaika na Bima hiii.
Anasema awali ilikuwa vigumu kwake kutibiwa hasa akikosa fedha za matibabu na hivyo kuhatarisha maisha yake.
" Niliteseka sana nilipopata ajali ya Pikipiki lakini baada ya kupata ushauri wa watalamu, Kadi ya Bima ilinisaidia kupata matibabu ya haraka na kupona haraka"
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa