Wilaya ya Rungwe inatajwa kuwa moja ya wilaya mkoani Mbeya ambayo mafanikio yake katika uwanja wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii umebebwa na uwingi wa maji yanayotiririka takribani kila kona.
Wilaya ya Rungwe inayopatikana chini ya kingo za safu za milima ya Uporoto ukiwepo mlima Rungwe wenye urefu wa 2,981 m.a.s.l na eneo lipatalo hekta 13,652.1 lenye msitu mnene unaowezesha kuhifadhi unyevunyevu na kuwa chanzo cha maji kwa sehemu kubwa.
Mlima Rungwe ni ukingo mwanana unawezesha kuziteka pepo zenye unyevunyevu toka ziwa nyasa (orographic rainafall) na kuliacha eneo hili kupata mvua takribani mwaka mzima huku upande wa pili wilayani Mbalali ukiachwa na ukame wa muda mrefu.
Afisa maendeleo ya jamii Bonde la ziwa Nyasa bibi Tumaini Mwalijeka anaiona fursa hii ya maji wilayani Rungwe kuwa ni lulu ambayo ikitumika vizuri wananchi watatoka katika maficho ya umasikini ambayo yanawaficha wakazi wengi bila sababu.
Bibi Mwalijeka anabainisha kuwa asilimia 59% ya maji ya ziwa nyasa yanatoka Tanzania ambapo huchangiwa na mito iliyopo wilayani Rungwe kama Mbaka, Kiwira, na Lufiliyo ambayo yote hutiririka toka Mlima Rungwe. Hii hutokana na mwegamo wa mwamba unaohifadhi maji chini ya ardhi (mpaka wa kihaidrojia) ambao hupelekea maji yote kuelekea upande wa wilaya Rungwe huku upande wa wilaya ya Mbeya vijijini,jiji na Mbarali kukiwa na vyanzo finyu na maji machache.
MAJI MAJUMBANI
Takribani wakazi wote wilayani Rungwe wanapata maji safi na salama. Meneja Mamlaka ya maji safi na salama katika mji wa Tukuyu anataja kuwa takribani wakazi wapatao 4560 sawa na asilimia 80% ya wakazi wote wanapata maji katika kata sita anazozihudumia huku akifafanua kuwa hata wakala wa maji vijijini (RUWASA) wakivifikia karibu vijiji vyote akiutaja mradi wa maji Masoko Group amabao umezinufaisha kata za Masoko, Kisiba , Bujela, na Itagata. Miradi mingine ni ile ya Ilolo na Kiwira.
Vijito vidogodogo vilivyoenea karibu maeneo yote hutumika kwa shughuli za umwagiliaji wa kilimo cha mbogamboga ambazo huuzwa katika masoko ya Kiwira, Tandale, Kyimo, Ikuti, Ntokela na maduka madodomadogo vijijini. Hali hii imeboresha kiwango cha uchumi wa kaya kwa wakazi walio wengi.
UTALII
Utalii wa maji ni wa kuvutia sana. Wengi hupenda kwa kuyaona, kuogelea, michezo ya majini kama diving na kutumia mitumbwi ya asili na boti za kisasa. Rungwe kwa kutumia vyanzo vyake vya maji zaidi ya alisilimia 90% hutumiwa kwa utalii. Mito kama Mbaka, na Kiwira ina mazingira mazuri ya kutalii kama daraja la Mungu na maporomoko ya Kaporogwe na Malasusa. Ziwa Masoko, na Ngosi ni zao la maji katika kukuza utalii. . Madaraja (viteputepu) vilivyopo takribani mito yote mikubwa ni utalii tosha. Daraja la STAMICO katika mto kiwira linalotenganisha wilaya ya Rungwe na Ileje ni kivutio cha pekee katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
USAFIRI.
Wakazi wengi hutumia maji kusafirishia mazao ya misitu kama mbao na magogo kutoka eneo moja hadi lingine. Hii hutokana na Mserereko wa maji uliopo hasa katika mito mikubwa ya Kiwira na Mbaka ambapo wakazi hutumia kusafiri kwa njia ya mitumbwi na huku wakiwa na mizigo yao kuelekea sokoni
UVUVI
Uwingi wa maji chini ya ardhi na mito mikubwa imewasaidia wakazi walio wengi kukupata kitoweo cha samaki ambacho hukutumia kama chakula cha kaya na ziada huiuza sokoni. Mabwawa makubwa yamejengwa karibu kona zote ambapo samaki wa kila aina wanafugwa na sasa wanasambazwa mkoani kote na nje ya nchi.
MAONI YA AFISA BONDE LA ZIWA NYASA.
Bibi Mwalijeka anawaomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kuendelea kutunza raslimali maji kwa kupanda miti rafiki kwa maji kutovitumia bila kibali kwani wanaweza kupata madhara kiafya bila kupata kibali na kupata ithibati maalumu. “ Kijani kinachoonekana Rungwe ni kutokana na uwepo wa maji ya kutosha chini ya ardhi na baadae mvukisho wake huchangia mvua kunyesha kwa wingi” aliongeza bibi Mwalijeka na kushamirisha kuwa maji hayatumiki tu kwa watu bali hata wadudu huyategea hivyo tuyatunze na kuyalinda.
NAMNA YA KUPATA KIBALI CHA KUTUMIA MAJI
IGharama ya fomu ya maombi ya kibali cha kutumia maji hutozwa kulingana na aina ya matumizi ya maji:
1. Maji kwa matumizi ya nyumbani ni kumiliki chanzo ni TZS 60,000/=
2.Umwagiliaji, ufugaji wa samaki, uzalishaji umeme, viwanda, biashara, kuendesha mitambo, na mradi mkubwa wa kusambaza maji kwa jamii ni TZS 250,000/=
3.Malipo yote hufanyika bodi ya maji ya Bonde la ziwa nyasa
4. BONDE huhudumia mikoa minne na wilaya kumi na tatu. Mkoa wa Songwe, Mbeya, Ruvuma na Njombe
5. Makao makuu yapo wilaya ya RUNGWE, Tukuyu mjini barabara ya Busokelo mkoani Mbeya
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa