Watalamu kutoka Bodi ya Maji Bonde la ziwa Nyasa @lakenyasabasin kwa kushirikiana na @halmashauri_ya_rungwe__mbeya wameendelea a zoezi la utoaji elimu dhidi ya utunzaji wa vyanzo vya maji katika maeneo mbalimbali
Leo Jumamosi tarehe 31.5.2025 imekuwa zamu ya kijiji cha Ibula kata ya Kiwira ambapo kupitia chanzo cha maji Katondo wananchi wamekumbushwa kuto fanya shughuli yoyote ya kibinadamu katika chanzo hiki ili kusaidia upatikanaji wa maji sambamba na usambazaji kuelekea kijiji cha Isaka kata ya Nkunga.
Wananchi wameelezwa kuwa kulima, kujenga makazi , kukata miti au kuchunga mifugo kando ya eneo la hifadhi ya chanzo hiki (Mita 60) kutadhofisha upatikanaji maji safi na salama sambamba na mazalia salama ya viumbe hai.
Chanzo cha maji Katondo kipo Magharibi kutoka shule ya Msingi Kibumbe ambayo imejengwa na kuzinduliwa na Mbio za Mwenge mwaka 2023
Uongozi wa Bodi ya Bonde la ziwa Nyasa utaanza zoezi la kuweka alama ( Vigingi ) hivi karibuni baada ya zoezi la kuwajengea uelewa wananchi kukamilika leo ambapo mamia ya watu wamejitokeza.
Chanzo cha maji Katondo kimekuwa tegemeo kwa wakazi wa ukanda wa chini wa kibumbe ambapo kwa kutumia nguvu za wananchi wamejenga banio kwa ajili ya kuanza usambazaji maji kuelekea katika kaya zao pamoja na kijiji cha Isaka ambacho tayari kinapata maji kupitia mradi wa maji Isaka ambao umekamilishwa na wakala wa maji vijijini (RUWASA)
l
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa