Bi.Ruth Masam Afisa Miradi Shirika la DSW Tanzania ameeleza kuwa kumlinda mtoto dhidi ya vikwazo mbalimbali na kumpa haki zake za Msingi ni hatua bora katika kuboresha maisha yake na kupanua ustawi bora wa jamii nchi nzima.
Hayo yameelezwa wakati wa siku ya Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika ambapo Kiwilaya yamefanyika katika shule ya Msingi katumba II.
Amesema Shirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo limeendelea kutoa elimu kwa jamii sambamba na kutoa ujuzi na maarifa ya namna bora ya kutokomeza ukatili kwa watoto katika jamii.
Shirika limeendelea kutoa mchango katika kuboresha maisha ya wananchi ambapo katika hatua hii limetoa vitabu, seti ya televisheni,na vifaa vya michezo katika shule mbalimbali na baadhi ya vikundi vya kijamii vijijini.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa