Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Polycarp Ntapanya ameomba viongozi wa Dini pamoja na wale wa Mila katika wilaya ya Rungwe kuendelea kuwa mstari wa mbele kutoa hamasa kwa jamii dhidi ya chanjo ya UVIKO 19 ikiwa ni hatua muhimu ya kupata kinga madhubuti dhidi ya virus vya Corona na hivyo kupata muda mzuri wa kushiriki shughuli za maendeleo na uzalishaji mali.
Hayo ameyasema wakati wa kikao maalumu cha watalamu wa afya pamoja na viongozi wa dini/ Mila kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri-Mwankeja ambapo pamoja na mambo mengine imearifiwa kuwa Halmashauri tayari imepokea jumla ya dozi 2000 za chanjo ya SNOPHARM.
"Kwa moyo wa dhati kabisa niwaombe viongozi wa mila na Dini nyie muna wafuasi wengi na wanawaamini, Mtusaidie! Ukianza kuchanja wewe nyuma yako itaondoa upotoshaji wote kama upo". amesisitiza bwana Ntapanya.
Aidha Bwana Ntapanya amesisitiza kuwa serikali ina lengo zuri kwa watu wake ikilenga kuwapatia afya bora na stahiki hivyo watu wajitokeze kupata chanjo hiyo ambayo inatolewa bure na serikali.
Dozi mpya ya Synopharm inaanza kutumika hivi karibuni ambapo mtu atachanjwa kwa awamu mbili moja baada ya siku 21 tofauti na ile ya Janseen Johnson ambapo mnufaika anadungwa kwa mara moja tu.
Katika wilaya ya Rungwe asilimia 97% ya dozi ya Johnson iliyopokelewa tayari imewafikia wanufaika na kudungwa na hivyo kupata kinga dhidi ya virus vya CORONA.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa