Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau (hayupo pichani) amenunua na kumpatia kompyuta mpakato(laptop) mwanafunzi Samwel Mwakamele kidato cha pili wa shule ya sekondari Kiwira ikiwa ni jitihada ya kurahisisha ujifunzaji kwa mwanafunzi huyo.
Kompyuta hiyo imegharimu kiasi cha shilingi laki 8.5
Mwanafunzi huyo mwenye ulemavu wa viungo ameshukuru msaada huo kwani utamsaidia kuandalia masomo yake na kujibia mitihani.
"Mkurugenzi huyu Mungu ambariki sana angeweza kuwapa watoto wake, lakini amenikumbuka mimi muhitaji kwa kweli namshuru sana" Ameongeza.
Hata hivyo mzazi wa mtoto huyo Bi. Itika Mwakamele amehamasisha wazazi wote Wilayani Rungwe kutowaficha watoto wenye ulemavu badala yake wawapeleke shuleni ili kuwajengea maarifa na ujuzi mbalimbali.
Samwel Mwakamele anaulemavu wa viungo ambapo hawezi kuandika kwa mikono lakini kompyuta hii inaenda kurahisisha ujifunzaji baada ya walimu wake kumfundisha namna ya kuitumia.
Awali Samwel alisoma shule ya msingi Mpandapanda na kufaulu kwa daraja C kisha alijiunga na shule ya Sekondari Mwakaleli kabla kuhamishiwa Kiwira.
BABA AMTOROKA MAMAMwaka 2006 baada ya Samwel Kuzaliwa baba yake mzazi alimtelekeza pamoja na mama yake mpaka sasa hajulikani alipo.
SHULE NA MAMA WAJENGA NYUMBA
Ili kumpunguzia Samwel kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya elimu, Mama yake Mzazi kwa kushirikiana na uongozi wa shule wamejenga nyumba ya makazi ambapo pamoja wote wataishi hapo huku akifuatilia maendeleo yake kwa karibu mpaka atakapohitimu elimu ya sekondari.
NAMNA ALIVYOHITIMU ELIMU YA MSINGI
Mkuu wa shule ya Sekondari Kiwira Mwal. Msafiri anaeleza kuwa mwanafunzi huyo alipewa mtihani wa kijieleza (oral examination) na hatua zingine aliandika mwenyewe na hivyo kupata ushindi hatimaye kuchaguliwa elimu ya sekondari.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa