Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau ametembelea shule ya sekondari Ndanto, Ndembela one na Bujinga na kisha kuzungumza na wafanyakazi wa shule hizo.
Pamoja na mambo mengine amesisitiza ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa vinavyoendelea katika shule hiyo kukamilika kwa wakati huku wakizingatia taratibu za ujenzi ili vidumu kwa muda mrefu na hivyo kutumiwa na kidato cha kwanza mwakani.
Aidha ameagiza kamati zote zinazotekeleza miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Wilayani Rungwe kuendelea kununua vifaa vya ujenzi mapema ili kuepuka changamoto ya kuadimika kufuatia miradi ya aina hii kutekelezwa nchi nzima.
Pamoja na hayo Bwana Mchau ameagiza Wakuu wa shule zote kubandika mpango kazi katika eneo la mradi ili kuwasaidia mafundi kurejea na kujipima spidi ya utekelezaji ambapo miradi yote inatakiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe inatarajia kutumia shilingi billion 1.1 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 55 vya madarasa katika shule za sekondari 18 kati ya 42 huku shule ufaulu wa wanafunzi elimu msingi kwa darasa la saba kiwilaya ukifikia asilimia 90.59% ongezeko la asilimia 5% ya ufaulu wa mwaka jana.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa