• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Rungwe District Council
Rungwe District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, U mwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafishaji na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Tehama na Mahusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Utunzaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Uzalishaji wa Maziwa
    • Kiwanda Cha Matunda
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Ardhi na Maliasili
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
      • Mikutano ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Katiba Pendekezwa
    • Mihutasari
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Matukio
    • Habari
    • Makala

DC RUNGWE ATEMBELEA VYOMBO VYA HABARI

Imewekwa Tarehe: February 22nd, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffar Haniu ametembelea vyombo vya habari vilivyopo  Wilayani Rungwe na kujionea vipindi mbalimbali vinavyorushwa vituo hivyo sambamba na kuzungumza na wananchi.


Vituo alivyotembelea ni pamoja na redio Rungwe na Chai  FM vyote vikiwa Tukuyu Mjini.


Katika vituo hivyo kwa nyakati tofauti Mhe. Haniu ameeleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali hivyo vyombo hivyo havina budi kuandaa vipindi vitakavyoelimisha jamii, kuhamasisha, kuikosoa na kuburudisha jamii.


Mhe.Haniu  ambaye kitaluma ni Mwanahabari, ameeleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuhamasisha watoto wote waliofikia umri wa kwenda shule kufanya hivyo mapema ili kuwawezesha kupata haki yao ya Msingi kwa Maendeleo na Ustawi wa taifa la Tanzania.


Ameeleza kuwa Tanzania kupitia Mradi wa Boost imeanza kuboresha miundombinu ya  kutolea huduma ya elimu ya Msingi ambapo Ujuzi kwa walimu, Vitabu, Vyoo na  madarasa yatajengwa.


Akizungumzia Sekta ya Kilimo, Mhe Haniu amesisitiza kuwa Serikali imeendelea kusambaza Mbolea ya Ruzuku kwa Wakulima Wilayani Rungwe  na kuonya Mawakala pamoja na  wakulima wanaouza na kununua Mbolea hiyo kwa njia ya udanganyifu kuacha kufanya hivyo kwani wanarudisha nyuma juhudi za Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwaletea Maendeleo wananchi Wake.


Aidha Mhe. Haniu  ameeleza kuwa Serikali imeendelea kuboresha masoko ya bidhaa mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara ndogondogo ( Wamachinga) ili kutoa fursa ya kujiongezea kipato Cha kila siku.


" Ndugu zangu wananchi niwambie, unapojengewa soko maana yake kumsaidia mteja ajue bidhaa ipi ataipata wapi. Vivyo hivyo wamachinga, soko la ndizi na bidhaa zingine Masoko haya yamesaidia sana likiwemo soko la Mwambenja lililofunguliwa Leo"


Mhe. Haniu ameagiza wafanyabiashara kufanya shughuli zao katika maeneo yaliyotengwa kwa nia nzuri ya kuboresha mandhari ya mji, Usafi wa mazingira, Mapato ya Serikali na Usalama wa Mali zao.


Katika hatua nyingine Mhe Haniu ameagiza wakazi wa Wilaya ya Rungwe kuacha migogoro ya ardhi na kuwa imekuwa ikihatarisha amani na utulivu katika Jamii.


Amesema Ofisi yake pamoja na Mabaraza ya ardhi amekuwa akitatua migogoro mbalimbali ya ardhi sambamba na utoaji  elimu dhidi ya Matumizi bora ya ardhi na kuandika Wosia kwa ngazi ya kaya hali itakayomaliza migogoro hiyo katika Wilaya ya Rungwe.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE SEMINA NAFASI YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR December 19, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA AKIBA NAFASI YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI December 19, 2024
  • TANGAZO BARAZA LA MADIWANI April 27, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MKATABA June 10, 2021
  • Onesha Vyote

Habari Mpya

  • BLAC MAENDELEO YAHITIMISHA MAFUNZO KWA WAKAZI WA WILAYA YA RUNGWE

    May 02, 2025
  • CHANJO YA POLIO KUTOLEWA MEI MOSI

    April 16, 2025
  • KAMATI YA SIASA YAPONGEZA MIRADI

    April 15, 2025
  • MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YAWANUFAISHA WANANCHI

    April 07, 2025
  • Onesha Vyote

Video

Vivutio vya Utalii
Picha Mjongeo Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • TAMISEMI

Vinganishi Linganifu

  • OR TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Ufundi
  • Sekretarieti ya Ajira Utumishi wa Umma

Kipimo cha Wateja Duniani

world map hits counter

Wateja Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB

    Sanduku la Posta: Box 148

    Simu: 025 255 2586

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Huruhusiwi
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa