Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu Leo tarehe 07.02.2023 amezindua vyumba sita (06) vya madarasa katika shule ya Msingi Kinyangwa iliyopo Kijiji Cha Katunduru kata ya Ilima.
Mradi wa ujenzi wa vyumba hivyo umetekelezwa na Kampuni ya Bioland kupitia Mradi wa Cocoa for Schools kwa garama ya shilingi million 64 huku wananchi wakichangia nguvu zao kwa zaidi ya shilingi Million 30.
Kampuni ya Bioland hujishughulisha na ununuzi wa zao la Kakao na faida yake huirejesha kwa jamii Kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Jumla ya kata 04 zinanufaika na Mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa ( Shule za Msingi) ambazo ni kata ya Masukulu, Matwebe, Ilima , na Kisiba huku shule ya Sekondari Masukulu ikijengewa Bweni la kisasa kwa ajili ya wasichana.
Akizundua madarasa hayo Mhe.Haniu ameishukuru Kampuni hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuwa kufanya hivyo itaongeza ufaulu katika shule hiyo baada ya mazingira ya kusomea na kujifunza kuboreshwa.
Amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha mazingira mazuri ya kufundishia hivyo wadau Mbalimbali pamoja na wananchi hawana budi kumuunga mkono sambamba kutunza miundombinu ya elimu ili ikinufaishe kizazi hiki na kijacho.
Mhe. Haniu ameagiza wazazi wote katika Kijiji hicho kujitokeza na kuchangia chakula Cha mchana shuleni ikiwa ni nyenzo imara ya kuongeza ufaulu sanjari na kuondoa udumavu na utapiamlo kwa watoto.
Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau ameeleza kuwa ufaulu kwa wanafunzi wa elimu ya Msingi umeendelea kupanda mwaka hadi mwaka kwa asilimia 93.7% (2022) na hii imechangia na Ufundishaji mzuri wa walimu, ubora wa miundombinu ya kufundishia na chakula shuleni.
Hata hivyo Bwana Mchau ameonya baadhi ya walimu kutumia muda wao vibaya badala ya kufundisha wanafunzi na hivyo kusababisha wanafunzi Kukosa maarifa na ujuzi hatimaye kushindwa mitihani yao ya mwisho.
Katika hatua nyingine Uongozi wa Kampuni ya Cocoa for School umeeleza kuwa utaendelea kuisaidia shule hiyo kwa kukarabati Ofisi ya walimu pamoja na vyumba vingine vitatu vya madarasa vilivyobaki.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imeahidi kuchangia ujenzi wa vyoo kwa ajili ya shule hiyo huku Ofisi ya Mbunge ikiahidi kuchangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa shule hiyo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa