DC HANIU ASHIRIKI ZOEZI LA UPIMAJI AFYA MAKANDANA
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe Jaffar Haniu ameshiriki zoezi la upimaji wa afya katika Hospitali ya wilaya Tukuyu Makandana.
Mhe.Haniu amefanya hivyo ikiwa ni sehemu ya Uhamasishaji wa wakazi wa Wilaya ya Rungwe kupima afya zao kufuatia uwepo wa Madaktari Bingwa waliopo katika hospitali hii.
Wataalamu hawa wa afya maarufu kama Madaktari Bingwa wa Mama Samia wameendelea na zoezi hili ambalo litadumu kwa siku tano na limeanza siku ya jumatatu mpaka ijumaa tarehe 17.5.2024
Mhe Haniu amempongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan na Wizara ya afya kwa ujumla kwa uamuzi huu mzuri kwani kufanya hivyo imewapunguzia wagonjwa kufuata huduma hii muhimu katika Hosptali ya Taifa Muhimbili na hivyo kutumia gharama kubwa.
Amesema wananchi katika wilaya nzima wanatakiwa kuchangamkia fursa hii adimu kwa ustawi bora wa maisha ya binadamu.
Kwa upande wa wananchi wameishukuru serikali kwa msaada huu uliotolewa.
Ndimbuni Kaburi Mkazi wa Kyimo ameifurahia huduma hii na kuwa amepata matibabu mazuri ikiwa ni pamoja na upasuaji.
Naye Haruna Asumwisye mkazi wa kata ya Lufingo ameipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuwaleta watalamu hawa huku akiomba siku ziongezwe ili kukidhi hitaji la wagonjwa wengi.
Kwa upande wake Mganga mkuu Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Dkt Diocles Ngaiza ametoa pongezi kwa serikali kwani ujio wa Madaktari Bingwa pi umesaidia kuongeza utalamu kwa wadumu wa afya katika hosptali yake na hivyo kujipatia ujuzi na maarifa mbalimbali ya kutibu wagonjwa.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa