Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe Jaffar Haniu ameboresha taarifa zake katika Daftari la kudumu la Mpiga Kura katika kituo cha Shule ya Msingi Madaraka Tukuyu Mjini.
Zoezi hili linalenga Uboreshaji na Kujiandikisha upya kwa wakazi waliofikia umri wa miaka 18 au ifikapo siku ya Uchaguzi mwakani 2025 atakuwa amefikisha umri wa miaka 18.
Aidha wale ambao vitambulisho vyao vimepotea au kuharibika au wamehama kutoka makazi yao ya awali wanayo fursa ya kupata kitambulisho hiki muhimu kwa Demokrasia na Maendeleo ya nchi hii.
Zoezi limeanza tarehe 27.12.2024 na linatarajiwa kuhitimishwa tarehe 2.1.2025
Jumla ya vituo 278 vimetapakaa katika vijiji vyote 99 ikinuia kutoa huduma karibu na wananchi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa