Mkuu wa wilaya ya Rungwe mhe. Nyangidu Julius Chalya amehani msiba katika kijji cha Goye kata Ndanto ambapo pamoja na mambo mengine mzee Lazaro Chaula (mfiwa) ameshukuru serikali kuwa karibu na watu wake kwani kwa kufanya hivyo inaleta mshikamano na ukaribu na watu wake.
Awali akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya Msingi Isyonje Mhe. Chalya amewaomba wakazi wa kijiji hicho kuendelea kujitolea michango ya ujenzi wa shule hiyo kwani kwa kufanya hivyo shilingi million 20 zilizotolewa na Mhe. Rais zitafanikisha ujenzi wa madarasa ya shule hiyo.
Akitoa takwimu Mhe. Chalya amesema kuwa katika kufanikisha ujenzi huo Shamba la miti Kiwira limetoa mbao, mchanga pamoja na madawati darasa moja huku ofisi ya Mkurugenzi halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ikitoa mifuko ya saruji na mawe ili kukamilisha ujenzi huo.
Wananchi watachangia Million 5 pamoja na nguvu kazi tu.Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa umeanza na unatarajiwa kuisha hivi karibuni.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa