Wakazi wa wilaya ya Rungwe wameombwa kuendelea kuchukua vitambulisho vya wajasiriamali kwa watendaji wa kata walio karibu na maeneo yao kwa lengo la kujihakikishia usalama wa biashara zao ikiwa ni pamoja na uwezo wa kukitumia mahali popote nchi nzima.
Mapema leo akiongea na watendaji wa kata 29 katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Julius Chalya amewaomba watendaji hao kuhakikisha hawawafumbii macho watu wote wanaofanya biashara bila leseni au kitambulisho.
Aidha mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter amewapa wiki moja watendaji wote kuhakikisha wamevigawa vitambulisho hivyo ili kuwapa urahisi wafanyabiashara kufanya kazi zao bila bugudha na hivyo kuepuka kulipa tozo zisizo za lazima na hivyo kukuza mitaji yao.
Kitambulisho kimoja hugawiwa kwa TZS 20,000/= na mpaka sasa kata ya SUMA, ILIMA, KINYALA, KISIBA NA MASUKULU (watendaji waliosimama) zinaongoza kwa kwa wakazi wao kuchukua vitambulisho kwa wingi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa