Chanzo ya Ugojwa wa Polio inatarajiwa kutolewa katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Kuanzia Mei Mosi mwaka 2025
Huu ni mfululizo wa chanjo ambapo imekuwa ikitolewa katika vipindi tofauti
Chanjo ya Polio hutolewa kwa watoto mara tu wanapozaliwa na kuendelea kutolewa mara wanapofikia umri wa miaka 6, 10 na 14
Lengo la chanjo hii ni kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa wa polio nchini.
Chanjo ya Polio hutolewa kwa watoto ikiwa ni nyenzo madhubuti ya kuwakinga na ugonjwa wa Kupooza.
Ugonjwa wa kupooza(Polio) huambukizwa na Virusi vijulikanavyo kwa jina la POLIOVIRUS
Ugonjwa huu unaweza kumpata mtu yeyote ila watoto huathirika zaidi.
Virusi vya Polio humwingia mtu kupitia chakula,au maji yaliyochafuliwa
Virusi vya ugonjwa huu hukaa kwenye utumbo wa binadamu na kuzaliana kwa haraka na baadaye hushambulia mishipa ya ufahamu
Mishipa ikiathirika huchoche sehemu au mwili mzima kupooza.
UTOAJI WA CHANJO KUANZIA MEI MOSI 2025
Chanjo itatolewa kupitia vituo vya kutolea huduma ya afya na ziara za Mkoba ambapo hutembelea kaya kwa kaya.
Watalamu wa afya wameendelea kushauri mtoto anapofikisha umri wa wiki 14 anatakiwa kupewa Dozi ya kwanza na Dozi ya Pili itolewe mara anapofikisha umri wa miezi 9
Habari hii na nyingine nyingi inapatikana kupitia www.rungwedc.go.tz
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa