Rungwe District Counci l .Diwani wa kata ya Kiwira Mhe. Klait Mwamwimbe amehamasisha wakazi wa kata ya Kiwira kuendelea kuchangia chakula shuleni ikiwa ni hatua muhimu ya kuongeza lishe kwa wanafunzi sambamba na kuongeza kiwango cha ufaulu.
kiwa katika mkutano wa wazazi shule ya msingi Ilundo Mwamwimbe ametaja kuwa uchangiaji wa chakula unaoendelea katika kata hiyo umesaidia kuongeza kiwango cha ufaulu na kwa kufanya hivyo kila mzazi anatakiwa kuhakikisha kuwa suala hilo linakuwa endelevu ili kuboresha afya bora ya watoto ili kutokomeza utapiamlo na udumavu katika kata hiyo.
Amesema katika msimu uliopita kata hiyo imeongoza katika ufaulu huku shule ya msingi Kiwira na Mpandapanda zikiongoza kufaulisha na kupeleka wanafunzi katika shule zenye vipaji maalumu kitaifa ambapo pamoja na mambo mengine hali hii imechangiwa na uhakika wa chakula cha mchana katika shule hizo.
"Malengo yetu ni kuhakikisha shule zote zinafanya vizuri na hili litawezekana iwapo kila mzazi atachangia chakula shuleni" Ameongeza.Mtendaji wa kata ya Kiwira Bwana Noel Mng'ong'o amearifu kuwa katika shule zote 12 za Msingi pamoja na sekondari 04 za Serikali , uchangiaji wa chakula shuleni umeazimiwa kuwa ni suala la lazima kwa kila mzazi na kushindwa kufanya hivyo Mzazi atalazimika kutoka mifuko 03 ya saruji ikiwa ni adhabu, saruji itakayosaidia kuboresha miundombinu ya shule.
Wakati huo huo Afisa Ustawi wa jamii Wilaya ya Rungwe Bi. Eliza Maembe ametaja kuwa Kushindwa kuchangia Chakula Shuleni kunapelekea wanafunzi hasa jinsia ya kike kujiingiza katika makucha ya ukatili wa kijinsia kwa kujiingiza katika makundi ya kupata njia mbadala ya kupata chakula na hivyo kupewa fedha na watu wasio stahili ili kuweza kujikimu kila siku na hivyo kusababisha kupata mimba za utotoni, kufukuzwa shule, na kupoteza ndoto zao za maishaZaidi ya asilimia 50% ya wanafunzi katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe (shule za msingi) hupata chakula cha mchana shuleni, hali hii imesukuma mbele matokeo ya mtihani wa taifa darasa la Saba 2021 ambapo Rungwe ilishika nafasi ya pili kimkoa kwa asilimia 90.6% huku shule za umma kama Kyimbila, Ndaga, Bagamoyo, Magereza, Kiwira, Mpandapanda, zikifanya vizuri zaidi