Noah Kibona, Rungwe Dc
Ufungaji wa mfumo wa kamera( CCTV) umekamilika na kuanza kufanya kazi katika hospitali ya wilaya Tukuyu (Makandana) ikiwa ni ahadi aliyoitoa Mkurungezi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter wakati akizungumza katika kipindi kinachorushwa na kituo cha Rungwe FM 102.5 Mhz. ambapo pamoja na mambo mengi alizungumzia mafanikio ya halmshauri ya wilaya ya Rungwe kwa miaka mine iliyopita.
Akizungumza hatua hiyo, Kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Dr.John Mrina amesema kuwa kamera hizo zitasaidia kuboresha usalama wa hosiptali ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma ya matibabu kwa wagonjwa.
Aidha Dr. Mrina ameongeza kuwa kwa sasa ufuatiliaji wa utoaji wa huduma kwa wagonjwa umeboreshwa kwani kwa sasa itakuwa rahisi kufuatilia malalamiko mbalimbali yanayotolewa na wagonjwa ikiwa ni pamoja na kubaini vitendo vinavyoharibu staha ya hospitali kama uchafuzi wa mazingira, na mambo mengine kadha wa kadha.
Hata hivyo kaimu mkuu wa kitengo cha TEHAMA halmashauri ya wilaya ya Rungwe bwana Frank Choka amewaomba watumiaji wa mfumo huo kuhakikisha wanautunza ipasavyo ili udumu kwa muda mrefu na kuleta tija kwa hamshauri na taifa kwa ujumla.
Kefa Mwakisuka ni mkazi wa kijiji cha Kyimo katika kata ya Kyimo tarafa ya Ukukwe ameusifu mfumo huo kwani utamhakikishia kupata matibabu ya uhakika na kuepuka malalamiko ambayo wakati mwingine yalikosa uhalali kutokana na kukosa uhalisia. “ hata nikisahau mali yangu pale hospitali itakuwa rahisi kubaini ni nani amechukua na ameelekea upande gani”. Aliongeza bwana Mwakisuka.
Pamoja na hayo katika moja vikao vya Baraza la madiwani, Mwenyekiti wa halshauri ya wilaya ya Rungwe Mh. Ezekiel Mwakota aliomba wagonjwa kuepuka kutoa malalamiko dhidi ya Hospitali hiyo hasa wanaposhauriwa na watalamu kuwa ugonjwa walioubaini hauwezi kutibiwa hospitalini hapo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na uwezo wa kutoa dawa kwa daraja la ugonjwa uliobainika.
Mh. Mwakota pia aliwaomba wagojwa kutibiwa katika zahanati zilizo katika maeneo yao ili kupunguza msongamano katika hospitali ya wilaya hasa kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibiwa katika vituo hivyo ambavyo vimesambaa katika vijiji na kata za wilaya hiyo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa