Shirika lisilo la Kiserikali la BLAC Maendeleo Kwa Kushirikiana na Master Card Foundation kupitia Mradi wa AIM (Accerelating Impact for young Women and Aidolescent Girls) wamehitimisha Mafunzo yao kwa Wahitimu 1500 kutoka katika kata Nne ndani ya Halmashauri ya Rungwe
Kata hizo ni pamoja na Mpuguso, Ilima, Msasani na Makandana
Wahitimu wamepewa vyeti ikiwa ni ishara ya kutambua ushiriki wao
Mradi Umelenga Kumwezesha Mwanamke kijana kuweza kujipatia kipato na hivyo kuepukana na hali ya utegemezi katika jamii.
Pia mradi umetoa mafunzo kwa vijana wa kiume ili kuleta usawa katika jamii.
Shirika hili lililoanza kutoa huduma yake kwa jamii toka mwaka 2024 limejijengea heshima kwa kutoa elimu ya ujarisiliamali kwa Wanawake na vijana, Ufugaji, Kilimo, Ufundi Stadi, Elimu ya Matumizi ya fedha na Mchanganuo wa Biashara.
Kupitia Elimu hii Wanawake wengi wamejikwamua katika Makucha ya Umasikini na hivyo kujipatia maeneo endelevu.
Haya yamethibishwa na Anana Kajela mkazi wa Makandana ambaye kutokana na elimu ya Biashara aliyopata amebahatika kuanziasha duka, Mgahawa na Ufugaji wa Nguruwe.
Naye Bi Anastazia Amanyisye Mkazi wa kata ya Ilima ameishukuru taasisi hii kwani alipoanza kupata mafunzo imemsaidia kupata uelewa dhidi ya Matumizi ya pesa hatua iliyomsaidia kuwa na bajeti nzuri ndani ya kaya yake
Nao Wanafunzi kutoka katika Shule ya sekondari Ilima wakiimba wimbo wao walishukuru shirika kwa kuwapa elimu balehe, kupambana na vitendo vya ukatili sambamba na namna ya kushiriki shughuli za uzalishaji mali shuleni na nyumbani.
Aidha Bi Agatha Mwega Meneja Mradi wa Blac Maendeleo ametaja kuwa Mradi umefanikiwa kuwezesha kiuchumi Wanawake 341 katika sekta zifuatazo
Kilimo 90
Ufugaji 97
Ufundi Stadi 30
Biashara ndondogo 124
Bi Agatha ameyataja Mafanikio yaliyopatikana ndani ya Mwaka mmoja kuwa ni pamoja Kufingua Clup space 12 ambazo zimesaidia wanawake na vijana balehe kujengeana uwezo na uelewa wa mambo mbalimbali ya uchumi na ustawi wa jamii
Aidha Kamati ya Maendeleo ya vijana (YDC) imeanzishwa kwa kushirikiana kwa kushirikiana na watendaji wa vijiji ambapo kuibua na kuwasaidia vijana katika changamoto mbalimbali.
Wanufaika wqmefundishwa kwa kutumia mtaala maalumu dhidi ya :
✓Namna bora ya kuishi na jamii na kuchagua marafiki wazuri
✓Namna bora na Sahihi ya kutunza fedha na kuwa na mchanganuo wa biashara
✓Namna sahihi ya kuibua na kupinga vitendo vya kikatili na kuripoti katika mamlaka husika ili kuvitokomeza
Village Saving Loan Associaon (VSLA) Ambvyo ni vikundi vya kuweka akiba na kukopeshana 17 vimeanzishwa na kubahatika kufikisha mtaji wa shilingi Million 6,312,000/=
Mradi pia umesaidia kuwaunganisha Wanufaika wa wafunzo na watalamu wa sekta ya kilimo, Mifugo na Maendeleo ya jamii ili kuwapa usaidizi katika shughuli mbalimbali za uzalishaji mali.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa