Kikao cha Baraza la Madiwani kwa robo ya nne mwaka wa fedha 2022/ 23 kimeketi leo tarehe 04 .8.2023.
Katika kikao hiki Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga ameeleza kuwa katika Kipindi hicho cha miezi mitatu kuanzia Mwezi Apri-June Halmashauri imekusanya kiasi cha Shilingi 1,744,352,376.61 sawa na asilimia 113.8% ya makisio ya Sh.1,532,865,000 ya kipindi hicho cha miezi mitatu.
Hata hivyo kuanzia mwezi Julai mwaka 2022 mpaka June 2023 (Mwaka mzima) jumla ya mapato yaliyokusanywa ni shilingi Billion 6,351,796,244.32 sawa na asilimia 104% ya makisio ya Mwaka mzima ya TZS Billion 6,131,460,000.00
Makusanyo hayo mazuri yametokana na Ushirikiano na Mshikamano mkubwa uliopo baina watumishi wa umma pamoja na wakazi wa Wilaya ya Rungwe na Tanzania kwa ujumla.
Mhe..Mwankuga ameeleza kuwa fedha za makusanyo zimesaidia katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Daharia (Hosteli) ya Wasichana katika shule ya sekondari Masukulu, Ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na zahanati, ukarabati wa machinjio na ulipaji wa stahiki mbalimbali za watumishi.
Aidha Baraza kwa pamoja limepitisha Azimio la Kumpongeza Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania kwa kuipatia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya ya Rungwe.
Fedha hizo zimesaidia katika Ujenzi wa kituo cha afya Iponjola, Kyimo na Ndanto.Aidha fedha hizo zimesaidia katika ujenzi na ukamilishaji wa vyumba vya madarasa na zahanati, barabara, maji na Umeme Vijijini.
Mathalani kupitia Mpango wa BOOST Serikali imetoa kiasi cha shilingi Million 970 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za msingi ikiwa ni pamoja uanzishwaji wa shule mpya tarajali ya Kibumbe kata ya Kiwira
Pamoja na hayo Serikali imetoa kiasi cha shilingi million 583 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari kata ya Lupepo, Million 100 ujenzi wa nyumba za walimu shule ya sekondari Msasani na Million 206 ujenzi wa Bweni na madarasa katika shule ya sekondari Wavulana Rungwe.
Katika kikao hiki Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe Ndg. Renatus Mchau ameliarifu Baraza kuwa Halmashauri imenunua vishikwambi kwa ajili ya uendeshaji wa Baraza kwa kila Diwani hatua itakayorahisisha shughuli za Baraza pamoja na kupunguza gharama ya ununuzi wa machapisho.
Katika hatua nyingine Baraza limepitisha jina Mhe.Samwel Mwakasege Diwani wa Kata ya Matwebe kuwa Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa kipindi cha mwaka 2023/24
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa