Mbele ya Kikao Cha Kawaida Cha Baraza la Madiwani kwa robo ya Kwanza kwa Mwezi Julai, Agosti na Septemba Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mhe.Mpokigwa Andimile Mwankuga amearifu kuwa katika kipindi hicho Halmashauri imepokea kiasi Cha Shilingi Million 654 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Fedha hizo zimeendelea kutumika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kutolea huduma kwa jamii.
Miundombinu hiyo ni pamoja na
1.Million 114 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya walimu Kyobo Sekondari.
2.Million 140 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Msingi Mpandapanda (Million 40) na Million 100 ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Msingi Goje.
3.Million 200 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili Kisondela Sekondari.
4. Million 200 kwa ajili ya ujenzi vyumba 10 vya madarasa kwa shule za Sekondari hii ikiwa ni kusaidia kwa wanafunzi watakaofaulu mtihani wa Darasa la Saba na kujiunga na kidato Cha kwanza 2023.
Aidha Katika kipindi hicho Halmashauri imekusanya kiasi Cha shilingi Billion 1,645,763,661.43 sawa na asilimia 107% ya makisio ya Shilingi 1,532,865,000.00.
Mapato hayo ni sawa na asilimia 27% ya makisio ya mwaka mzima ya Shilingi Billion 6,131,460,000.00
Mapato hayo yametoka na vyanzo vifuatavyo: Ushuru wa mazao, Mapato kutokana na Hisa, Leseni na ushuru mbalimbali, ada ya ushuru, Mapato kutokana na Mali za Halmashauri,ICHF na ada za shule, ushuru kutokana na Mali asili.
Mapato hayo yamesaidia uboreshaji wa vituo vya kutolea huduma kama elimu na afya pamoja na shughuli zingine za utawala.
Awali Jana katika Kikao Cha Baraza la Kazi Mhe.Mwankuga aliagiza WATENDAJI wa kata zote 29 wakishirikiana na Waheshimiwa Madiwani kuendelea kukusanya mapato kwa kasi na weledi na kuzuia mianya yote inayochangia watu wasio waaminifu kutorosha mapato ya Serikali.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa