Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe yapitisha Rasimu ya mapendekezo ya Mpango wa Bajeti kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020, Rasimu hiyo iliyowasilishwa na Afisa Mipango wa Wilaya ya Rungwe Bi.Husana Toni. Nakueleza kuwa Rasimu hiyo imezingatia vipaumbele vya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kama vifuatavyo: Kuboresha miundombinu ya Elimu ,Afya na Maji, Kuhamasisha wananchi na vikundi kujenga viwanda vidogo, vya kati na vikubwa , Kuweka mazingira ya Wilaya safi kwa kuzoa taka zinazozalishwa katika masoko, kuboresha miundombinu ya biashara na masoko ili kujenga mazingira mazuri ya biashara na ukusanyaji wa mapato, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa ngazi zote ili kukuza uwajibikaji, kushirikiana na wadau wa nje na ndani ya Halmashauri katika shughuli za maendeleo ili kukuza mahusiano na sekta binafsi, wananchi na wadau wa maendeleo, Kuboresha mazingira ya uwekezaji Wilayani kwa kuboresha miundombinu ya uwekezaji ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na jamii. Rasimu hiyo imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo (i) Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 Ambayo ilionesha mchanaganuo wa Vyanzo vya mapato,Makisio ya mwaka 2017/2018, jumla ya kiasi kilicho pokelewa Julai,2017-Juni, 2018 na asilimia ya mwaka husika.
Katika utekelezaji wa Mpango wa Bajet i ya mwaka 2017/208 Halmashauri ilipata mafanikio na changamoto kadhaa ambazo ziliongeza ufanisi /ubunifu katika utendaji kazi na kutoa huduma bora za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.
(ii)Mapitio ya Mpango na Bajeti wa mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kufikia mwezi Disemba 2018.
Kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilipanga kukusanya na kutumia kiasi cha tsh 46,307,163,194.48 hadi kufikia mwezi Disemba 2018 Halmashauri imepokea kiasi cha
tsh 21,121,982,745.85 sawa na 46% ya makisio yote. Utekelezaji wa miradi unaendelea kufanyika kulingana na mapokezi ya fedha za miradi hiyo. Aidha ,uhamisishaji unaendelea kufanyika kwa Wananchi na Wadau wengine wa maendeleo.
(iii)Rasimu ya mapendekezo ya Mpango na Bajeti kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/2020 imezingatia mambo mbalimbali ya muhimu ambayo ni Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, mwongozo wa kitaifa wa uundaji wa mipango na bajeti kwa tasisi za Serikali, Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015-2020, mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2018/2019, Ushauri na Mipango kutoka kwenye Kamati za Maendeleo ya Kata (KAMAKA), Viwango vya ukomo wa bajeti vilivyotumika katika mwaka 2018/2019 na mpango mkakati wa Halmashauri wa miaka mitano kuanzia 2015/2016-2019/2020.
Aidha Afisa Mipango alieleza kwamba katika mwaka wa fedha 2019/2020, Halmashauri inategemea kukusanya na kutumia kiasi cha Sh 48,364,443,782.00, vyanzo vya mapato ni Serikali Kuu, Mapato ya ndani na WahisanAidha mwenyekiti wa Halmashauri ameeleza kuwa Rasimu ya mapendekezo ya mpango na bajeti ya 20191/2020 imelenga kutekeleza huduma za jamii kwa wananchi kwaajili ya kupata mendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla alisema "kama Taifa litafanya uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya huduma za afya tutajikuta tunafanya mapinduzi makubwa sana katika miundo mbinu ya elimu na maji."
Picha ya Kwanza ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mh.Ezekiel Mwakota (mwenye skafu ya njano) akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi.Loema I.Peter (mwenye Skafu ya bluu) wakiwa na Katibu wa Umoja wa Wanawake (UWT) Rungwe katika mkutano wa Baraza Maalum.
(Pichani ni Baadhi ya madiwani na wakuu wa idara wakiwa katika Mkutano maalumu wa Baraza la Kupitisha Mapendekezo ya Rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020)
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa