Baraza la Kazi Madiwani limefanya mkutano wake wa kawaida tarehe 27/02/2019 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Mkutano huo ulijadili taarifa mbalimbali za maendeleo katika kata za Wilaya ya Rungwe pamoja na taarifa ya kata ya ambazo hazikukusanya vizuri mapato ya ndani na kutofikia asilimia 50 kwa robo ya pili kuanzia mwezi oktoba hadi disemba 2018.
Katika kujadili taarifa za maendeleo katika kata ambazo ziliwasilisha taarifa zake katika Mkutano huo wa Baaza la kazi, Kata ya Ibigi taarifa iliwasilishwa na Diwani wa Kata hiyo Mh.Lusubilo Simba.
Katika taarifa ya kata jiyo hiyo iliyo ilieleza mambo ya utawala bora, taarifa ya mapato na matumizi, miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika kata, ulinzi na usalama, afya na utunzaji mazingira, elimu, kilomo na mifugo na changamoto mbalimbali katika kata.
Aidha Kata ya Ibigi ina miradi mitano (5 ) ya maendeleo inayotekezwa katika kata ambayo ni miradi wa maji Katumba -Tukuyu wenye gharama ya 387,334,410/= chanzo cha fedha ni Serikali Kuu na miradi huu bado haujakamilika.Mradi wa ujenzi wa barabara solo mjinga-mafulasopo, utengenezaji wa madawati 144 shule ya sekondari Lupoto wenye gharama ya tsh 10,080,000/= chanzo cha fedha ni nguvu za wananchi,miradi wa nne ni ujenzi wa kituo cha afya ambao unatarajiwa kuanza kujengwa kwa sasa wananchi wameshaandaa eneo hilo kwa kulisafisha.Miradi mwingine ni ukarabati wa madatasa while ya msingi Katumba 1ambao una gharama ya 1,500,000/= chanzo cha fedha ni EP4R na sasa ujenzi huo upo hatua ya kupaua.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa