Baraza la madiwani la kazi limeketi leo katika ukumbi wa halmashauri - MWANKENJA. Pamoja na mambo mengine watendaji wa Kata, na vijiji wamehimizwa kuitisha vikao na mikutano Mara Kwa Mara ili kuwapa fursa wananchi kujua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali hii ikiwa ni pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali inayotolewa na serikali.
" Vikao ni jukwaa la mijadala na kujengeana ufahamu ambapo viongozi hutoa maelekezo ya serikali na wananchi kutoa kero zao na kutatuliwa Mara moja" amesisitiza Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga.
Aidha imearifiwa kuwa wananchi wanatakiwa kuwa na vyoo bora ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko ambapo afisa Mazingira na Usafi halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Salumu Kilanga ametoa sifa za choo bora kuwa ni pamoja na:
1. Kuwa na sakafu imara ili kuruhusu kusafisha Kwa urahisi.
2. Paa lisiloruhusu kuvuja
3. Mlango imara unaofungwa na kufunguliwa ili kuepusha wadudu kuingia na kutoka nje ya choo.
4. Maji Kwa ajili ya usafi ndani ya choo.
5.Kuta zijengwe Kwa tofari ili kuongeza uimara.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa