Baraza la Wafanyakazi katika Halmashauri ya Rungwe limeketi leo tarehe 16.1.2025 likijadidili rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/ 2026
Baraza hili hujumuisha viongozi mbalimbali kutoka vyama vya wafanyakazi pamoja na watalamu mbalimbali
Baraza pamoja na mambo mengine limeshukuru mafanikio yaliyofikiwa kwa mwaka wa fedha 2024/ 25.
Mafanikio hayo ni pamoja na kupandisha vyeo jumla ya watumishi 851 huku watumishi 179 wakipata ajira katika Halmashauri
✓Upatikanaji wa dawa na vitendanishi umefikia mpaka asilimia 95% katika vituo vyote vya kutolea huduma
✓Aidha jumla ya vituo 03 vya vya afya (Kinyala, Iponjola na Ndanto) Vimefunguliwa na hivyo kufikisha vituo 09 huku kituo cha Kiwira, Masoko, Malindo na Masebe ujenzi wake ukiendelea.
✓Halmashauri imefungua shule Mpya mbili za sekondari (Lupepo na Isaka) pamoja na tatu za msingi (Umoja, Ushirika na Chifu Mwanjali)
✓Pia imefanikiwa kujenga mabweni mawili katika shule ya sekondari Kisondela , Moja katika shule ya Lupoto , Rungwe , Tukuyu na Masukulu.
✓Ufaulu kwa darasa la saba umeongezeka kutoka aasilimia 93.2% mwaka 2022 mpaka asilimia 95.5% mwaka 2023
-Kidato cha nne kutoka asilimia 94% mwaka 2022 mpaka asilimia 95% mwaka 2023
-Kidato cha sita kutoka asilimia 99.09% mwaka 2022 mpaka asilimia 100 mwaka 2023.
✓Halmashauri imeweza kukusanya Mapato ya ndani kiasi cha shilingi 7,427,096,607.30 sawa na asilimia 103 ya makisio yaliyowekwa ya shilingi 7,179,615,400.00
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa