Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami umbali wa km 7 kuanzia Tukuyu Mjini mpaka Ntandabala (Pakati) umefikia hatua nzuri.
Barabara hii ni chipukizi mwanana katika uchumi kwa Halmashauri ya Rungwe na Busokelo zote zinazounda wilaya ya Rungwe.
Kumalizika kwa barabara hii kutafungua fursa za uwekezaji katika sekta ya kilimo, mifugo, Viwanda, elimu, afya, misitu, na usafirishaji.
Haya ni mafanikio makubwa kwa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Watu wake wanasafirisha mali zao hasa bidhaa za kilimo na viwandani kwa wakati na hivyo kuinua kiwango cha uchumi kwa ngazi ya kaya na taifa kwa ujumla.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa