Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rungwe Ndugu Mekson Mwakipunga ameongoza Kamati ya Siasa Wilaya katika uzinduzi wa barabara ya Ibililo -Kyosa yenye urefu wa km 10 kwa gharama ya shilingi Million 600.
Kwa sasa katika hatua ya kwanza itajengwa kwa umbali wa Km 04.
Barabara hiyo inatekelezwa na Wakala wa Barabara Vijijini na mjini (TARURA)
Akizindua barabara hiyo ndugu Mwakipunga ameishukuru serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi hicho cha fedha na kuwa barabara hiyo itafungua fursa za kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo hasa wakulima wa ndizi, kahawa na Iliki pamoja na mazao ya misitu
Ameeleza kuwa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo kila pembe na kwa hatua hii Mhe.Rais atajjizolea kura za ndiyo kwa kila mkazi wa wilaya ya Rungwe.
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe.Jaffar Haniu amewaagiza wakazi wa kijiji cha Ibililo pamoja na Kyosa kuhakikisha wanatunza vifaa vya Mradi, Kujiepusha na uhujumu sambamba na kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi na kuwa kushindwa kufanya hivyo mradi hautakamilika kwa wakati.
Mradi unatarajia kukamilika kwa muda wa miezi miwili kuanzia leo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa